Friday, September 7, 2007

Mwana wa Adam na maisha

Namshukuru mwenyezi Mungu kwa kunipa nguvu na akili inayonifanya niishi vizuri hapa duniani kwani yeye ndiye mpaji wa vyote,hasa nikiangalia ni wengi wameshindwa kuishi kama mimi ninavyoishi,wala sio kama mimi ni mwema sana kuliko wao bali ni baraka zake yeye aliye juu.hivyo basi nina kila sababu ya kumshukuru.

Ndugu zangu Maisha ni kama vita,tena vita tunayopigana bila kumuona adui, hii ni hatari sana kwani ni rahisi kwa adui kukuvamia na hatimaye kukumaliza,ukweli wa kumwogopa Mungu hakuna hata mmoja asiye taka kuwa na maisha bora na ya kifahari, hapa na maanisha kuwa na nyumba nzuri ya kuishi,gari la kutembelea, account iliyojaa pesa unazoweza kuzitoa bila mawazo,kuwa na familia yenye amani na inayomjua mungu,kazi inayokuingizia pesa mingi inayoweza kukutosheleza mahitaji yako wewe na wanaokuzunguka na nyingine uweze kuweka akiba.katika kutimiza hayo yote mtu anatakiwa kufanya kazi kwa bidii.
Kufanya kazi kwa bidii ni nini? Watu wengi wanashindwa kuelewa,kufanya kazi kwa bidii haina uhusiano na kazi zisizo rasmi kama wizi,rushwa na udanganyi hapa utakua umekwenda kinyume na taratibu na sheria za nchi,ndugu zangu naomba tuelewe kua kazi ni kazi bora mkono uende kinywani lakini kazi hizo lazima zitambulike na kukubalika katika jamii.

Siku zote tunasikia watu wanauwana sababu ya pesa,wengine wanafungwa sababu ya kujishughulisha na biashara haramu kama madawa ya kulevya hawa wote wanatafuta pesa ambazo ni msingi wa maisha bora kwani ukiwa na pesa teyari wewe unaheshimika katika jamii,lakini sasa mimi najiuliza kila siku hivi kwanini mtu anadiriki kutoa uhai wa mwenzake sababu ya pesa? Hivi mtu huyu anatambua uwepo wa Mungu kweli? Maana kama anajua kweli Mungu yupo asingethubutu kutoa uhai wa mwenzake, kwani Mwenyezi Mungu ametuhasa katika amri zake kumi yakua tusiue,iweje leo hii mtu huyo aende kinyume na amri hiyo? Mzee kituturu nisaidie.

Kimsingi lazima tukubaliane kuwa watu wengi wanajipatia mali zao katika njia ambazo zisizo halali,wengi wanakwenda kwa kalumanzira ambapo uwataka waue au wawafanye wenzao mazezeta,mimi naamini kabisa utajiri wa halali ni ule ambao haujavuka mipaka kwamaana ya kwamba upo katika standard inayokubalika,sasa hapa kiwango ni kipi naomba tusijadili hapo,hauwezi kuwa malt millionaire kwa kazi za kuajiriwa,na hata kama ni kujiajiri basi you must be blessed,ingawa mara chache watu kama hawa wanatokea.Egidio unasemaje hapo?

Swali la kujiuliza hapa ni kwanini utake mali ambazo kimsingi zitakuletea matatizo? Na je turudi kwenye vitabu vya dini,vinatuhasa nini kuhusu utajiri? Mungu aliona mbali sana na kutambua kua ni rahisi kwa Ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuuona ufalme wa mbinguni,wewe unafikiri hapa Mungu anamaanisha nini? Kama nilivyokwisha waeleza kua huwezi kuwa malt-millionare kwa njia za halali,ndio maana inakua vigumu kwa tajiri kuuona ufalme wa mbingu kwani lazima atakua ametenda maovu mengi sana ili kuupata utajiri alionao.hapa naomba mnielewe kua sisemi kwamba ni vibaya kuwa na utajiri,swala hapa ni kwamba utajiri wako umeupata namnagani? Je umeua? Au Umedanganya ilikupata uo utajiri?
amakweli Adam ameturithisha azabu kubwa sana ya kutafuta kwa jasho.

Maisha ya kumjua Mungu ni matamu sana! Namafanikio mazuri hayaji kwa njia yeyote isipokua kwa njia ya Mungu baba, rejea mithali 16 mstari wa nne unasema (mkabidhi bwana kazi zako na mawazo yako yatathibitika) najua utakua na maswali mengi sana ya kujiuliza juu yangu,wapo watakaosema jamaa siku hizi kaokoka nini? Mbona anajifanya anajua mambo ya Mungu sana? Wengine watasema kama kumjua Mungu ndio mafanikio mbona yeye hana? Na je tangu amjue huyo Mungu amefaidika na nini? Ukinijia na maswali kama hayo nitakujibu kwa kifupi tu! “Kwa Mungu hakuna haraka” pia nitakuuliza je mafanikio unayonihitaji niwe nayo ni yapi? Maana mpaka nilipo sasahivi ni mafanikio tosha hasa nikiangalia wanaohitaji kua kama mimi ni wengi lakini kwao ni vigumu,pia nitakwambia mwomba mungu hachoki! Ipo siku isiyo na jina wala tarehe mambo yatakua kama ninavyomwomba Mungu.rejea Luka 18:1-7.

Labda kikubwa hapa watu wasichotaka kuelewa ni juu ya IMANI,mtu ukiwa na imani juu ya mambo uliyomwomba Mungu lazima utafanikiwa kwani Mungu anajibu maombi yetu kwa njia kuu tatu,Mungu anaweza sema NDIYO na akakupa kile unachotaka,anaweza akasema HAPANA akakupatia kingine kizuri zaidi ya unachokitaka au akasema SUBIRI akakupa unachokitaka kwa wakati anaopenda yeye mwenyewe,ndugu zangu yatupasa tuelewe kuwa Mungu anaweza! hata maandiko yanasema kwamba ukimtegemea Mungu nae atakutegemeza.

Ni kawaida katika tamaduni zetu kuomba mungu na pia wapo wanaoamini kua mizimu inafanya kazi kwani wapo wanao omba mizimu kwa kuchinja mbuzi na kutoa kafara mbalimbali ili kuleta mafanikio katika maisha yao hasa wachaga,ukiwaambia watu hawa kuwa wanachokifanya ni zambi watakwambia hata kipindi cha kina Musa kulikua na kafara,Hapana! wazee wetu walikua wanatoa matoleo yao kwa Mungu na wala sio kwa mizimu.siku zote tambua kua Mungu hapaswi kuchanganywa na miungu wengine kwani hilo ametuasa katika amri yake ya kwanza kuwa tumwabudu mungu wetu na tusiabudu miungu wengine.

Tuame katika mada hiyo na turudi katika watu hawa wanaotoa roho za watu kwa ajili ya utajiri na kipekee kabisa tuzungumzie mtu unaye mpenda anapokufa.unajua ni kwanini nimezungumzia swala hili? Sababu mara nyingi watu wanaouliwa walikua ni vipenzi vya watu.wewe unafikiri watu hawa wanao uliwa mwisho wake ni nini?Je unafikiri damu za watu hawa waliouliwa wataacha kukuandama katika maisha yako? Je unafikiri kilio cha ndugu zake walioachwa wapweke kitaanguka chini bila kukuzuru? Hakika nakwambia hautaishi kwa raha hata siku moja kwani hakuna dhambi kubwa kama ya kuua.

Ebu fikiria umemuuwa kijana ambae ameoa karibuni,ni majonzi kiasi gani umesababisha kwa mke wake? Ebu jaribu kuwaza mzazi wako anauwawa wakati ukiwa form one nayeye ndio pekee unae mtegemea katika shule? Wewe unafikiri kilio cha watu hawa kitakuacha? Mzee chemsha bongo hayo mambo ni ya kawaida sana kule ukweni kwenu(upareni).
Sasa nini tufanye naacha swali hilo kwa wanablog mulijadili bila kusahau
Maandiko matakatifu ya mungu yanasema
usimuhukumu mwenzio kwani na wewe pia utaukumiwa kwa kipimo hichohicho.


Wakati mwingine tena wazee.

No comments: