Wednesday, September 12, 2007

AND HOW ABOUT THIS ONE

There is no chagga tribe but just different groups of people living around that mountain of Kilimanjaro with the following characteristics:

WASIHA: they are too backward,hawakwenda shule bado wanavuta ugoro kama wamasai,wanaume wanatahiriwa nusu!! Chaa achana nao.

WAMACHAME:huwezi kujua nani mwanamke na nani mwanaume,kila kitu ni pesa.yaani hata kama ni mkeo wa ndoa inakua hivi,’kama huto pesa ya mbege ndoa yangu sikupi babangu’basi kule Machame chakula cha ndoa(mapenzi) ni kwa kipimo,ukiwa katikati mama anakwambia stoooop! Hapo shilingi hamsini zako ndio zimekwisha,ukitaka ongeza uendelee.

WAKIBOSHO:specialized bandits,akina mama wakiwa wanatoa soga na mwenzie utawasikia hivi” yaani dadangu we acha Alex wangu siku hisi amepefuka kweli,ana akili we acha tu! Haibi tena mfukoni siku hisi ameunda kundi lake la ujambasi,krismasi ikifika lazima nitaletewa fitenge fya kongo” ladies likewise AKIOLEWA NA KYASAKA baba na mama wanamwambia hivi” hivi wewe huyu mwanaume kwani ni ndugu yako? Leta hizo pesa sake tujenge huku kwetu manka”!!

WAURU:very boring people,wakikaa ni kuongea kuhusu shule tuuuuu,masomo,digrii yaani Yukon not bilivu!Babu wa miaka 70 bado madaftari yake ya primary ameweka sandukuni!! Atawaonyesha wajukuu zake,ona hand writing yangu ilivyo nzuri wakati nafundishwa na father Wilson payatt.wanakumbuka majina ya walimu wao hasa wazungu tangu chekechea.wanamwogopa sana Mungu,kengele ya Kanisani ikilia saa sita utawaona wazee wote kilabuni wanasimama na kusali sala ya mchana ndio wanaendelea kunywa mbege.

WA OLD MOSHI:actually Mama Mkapa ni beaty queen kule kwao.yaani mimi sisemi nenda kachague wewe mwenyewe.wanaume ni wabishi balaa1 wanakunywa kisusio cha Nguruwe!! Na Gongo nyingiiiiiiiiii!

WAMARANGU:wanaume wote ni waongo.actually kuna somo la jinsi ya kudanganya shule zote za primary kule Marangu.both wanaume na wanawake maisha ni raha tupu.kwa Mmarangu halisi,kwanza ananunua gari,anachapa maisha,nae kulala kwenye gari wakati kodi ya nyumba inamshinda ni jambo la kawaida.

WAROMBO:kazi mtindo mmoja! Wanawake tunawaita KUBOTA aina ya matrekta yaliyosambazwa Kilimanjaro na wajapani,watafutaji wa pesa!!!! We acha tuu,lakini ukimchezea anakuua na kukimbilia kenya.


Wazee hayo ni baazi ya matabaka ya wachaga

tuonane wakati mwingine

Friday, September 7, 2007

Mwana wa Adam na maisha

Namshukuru mwenyezi Mungu kwa kunipa nguvu na akili inayonifanya niishi vizuri hapa duniani kwani yeye ndiye mpaji wa vyote,hasa nikiangalia ni wengi wameshindwa kuishi kama mimi ninavyoishi,wala sio kama mimi ni mwema sana kuliko wao bali ni baraka zake yeye aliye juu.hivyo basi nina kila sababu ya kumshukuru.

Ndugu zangu Maisha ni kama vita,tena vita tunayopigana bila kumuona adui, hii ni hatari sana kwani ni rahisi kwa adui kukuvamia na hatimaye kukumaliza,ukweli wa kumwogopa Mungu hakuna hata mmoja asiye taka kuwa na maisha bora na ya kifahari, hapa na maanisha kuwa na nyumba nzuri ya kuishi,gari la kutembelea, account iliyojaa pesa unazoweza kuzitoa bila mawazo,kuwa na familia yenye amani na inayomjua mungu,kazi inayokuingizia pesa mingi inayoweza kukutosheleza mahitaji yako wewe na wanaokuzunguka na nyingine uweze kuweka akiba.katika kutimiza hayo yote mtu anatakiwa kufanya kazi kwa bidii.
Kufanya kazi kwa bidii ni nini? Watu wengi wanashindwa kuelewa,kufanya kazi kwa bidii haina uhusiano na kazi zisizo rasmi kama wizi,rushwa na udanganyi hapa utakua umekwenda kinyume na taratibu na sheria za nchi,ndugu zangu naomba tuelewe kua kazi ni kazi bora mkono uende kinywani lakini kazi hizo lazima zitambulike na kukubalika katika jamii.

Siku zote tunasikia watu wanauwana sababu ya pesa,wengine wanafungwa sababu ya kujishughulisha na biashara haramu kama madawa ya kulevya hawa wote wanatafuta pesa ambazo ni msingi wa maisha bora kwani ukiwa na pesa teyari wewe unaheshimika katika jamii,lakini sasa mimi najiuliza kila siku hivi kwanini mtu anadiriki kutoa uhai wa mwenzake sababu ya pesa? Hivi mtu huyu anatambua uwepo wa Mungu kweli? Maana kama anajua kweli Mungu yupo asingethubutu kutoa uhai wa mwenzake, kwani Mwenyezi Mungu ametuhasa katika amri zake kumi yakua tusiue,iweje leo hii mtu huyo aende kinyume na amri hiyo? Mzee kituturu nisaidie.

Kimsingi lazima tukubaliane kuwa watu wengi wanajipatia mali zao katika njia ambazo zisizo halali,wengi wanakwenda kwa kalumanzira ambapo uwataka waue au wawafanye wenzao mazezeta,mimi naamini kabisa utajiri wa halali ni ule ambao haujavuka mipaka kwamaana ya kwamba upo katika standard inayokubalika,sasa hapa kiwango ni kipi naomba tusijadili hapo,hauwezi kuwa malt millionaire kwa kazi za kuajiriwa,na hata kama ni kujiajiri basi you must be blessed,ingawa mara chache watu kama hawa wanatokea.Egidio unasemaje hapo?

Swali la kujiuliza hapa ni kwanini utake mali ambazo kimsingi zitakuletea matatizo? Na je turudi kwenye vitabu vya dini,vinatuhasa nini kuhusu utajiri? Mungu aliona mbali sana na kutambua kua ni rahisi kwa Ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuuona ufalme wa mbinguni,wewe unafikiri hapa Mungu anamaanisha nini? Kama nilivyokwisha waeleza kua huwezi kuwa malt-millionare kwa njia za halali,ndio maana inakua vigumu kwa tajiri kuuona ufalme wa mbingu kwani lazima atakua ametenda maovu mengi sana ili kuupata utajiri alionao.hapa naomba mnielewe kua sisemi kwamba ni vibaya kuwa na utajiri,swala hapa ni kwamba utajiri wako umeupata namnagani? Je umeua? Au Umedanganya ilikupata uo utajiri?
amakweli Adam ameturithisha azabu kubwa sana ya kutafuta kwa jasho.

Maisha ya kumjua Mungu ni matamu sana! Namafanikio mazuri hayaji kwa njia yeyote isipokua kwa njia ya Mungu baba, rejea mithali 16 mstari wa nne unasema (mkabidhi bwana kazi zako na mawazo yako yatathibitika) najua utakua na maswali mengi sana ya kujiuliza juu yangu,wapo watakaosema jamaa siku hizi kaokoka nini? Mbona anajifanya anajua mambo ya Mungu sana? Wengine watasema kama kumjua Mungu ndio mafanikio mbona yeye hana? Na je tangu amjue huyo Mungu amefaidika na nini? Ukinijia na maswali kama hayo nitakujibu kwa kifupi tu! “Kwa Mungu hakuna haraka” pia nitakuuliza je mafanikio unayonihitaji niwe nayo ni yapi? Maana mpaka nilipo sasahivi ni mafanikio tosha hasa nikiangalia wanaohitaji kua kama mimi ni wengi lakini kwao ni vigumu,pia nitakwambia mwomba mungu hachoki! Ipo siku isiyo na jina wala tarehe mambo yatakua kama ninavyomwomba Mungu.rejea Luka 18:1-7.

Labda kikubwa hapa watu wasichotaka kuelewa ni juu ya IMANI,mtu ukiwa na imani juu ya mambo uliyomwomba Mungu lazima utafanikiwa kwani Mungu anajibu maombi yetu kwa njia kuu tatu,Mungu anaweza sema NDIYO na akakupa kile unachotaka,anaweza akasema HAPANA akakupatia kingine kizuri zaidi ya unachokitaka au akasema SUBIRI akakupa unachokitaka kwa wakati anaopenda yeye mwenyewe,ndugu zangu yatupasa tuelewe kuwa Mungu anaweza! hata maandiko yanasema kwamba ukimtegemea Mungu nae atakutegemeza.

Ni kawaida katika tamaduni zetu kuomba mungu na pia wapo wanaoamini kua mizimu inafanya kazi kwani wapo wanao omba mizimu kwa kuchinja mbuzi na kutoa kafara mbalimbali ili kuleta mafanikio katika maisha yao hasa wachaga,ukiwaambia watu hawa kuwa wanachokifanya ni zambi watakwambia hata kipindi cha kina Musa kulikua na kafara,Hapana! wazee wetu walikua wanatoa matoleo yao kwa Mungu na wala sio kwa mizimu.siku zote tambua kua Mungu hapaswi kuchanganywa na miungu wengine kwani hilo ametuasa katika amri yake ya kwanza kuwa tumwabudu mungu wetu na tusiabudu miungu wengine.

Tuame katika mada hiyo na turudi katika watu hawa wanaotoa roho za watu kwa ajili ya utajiri na kipekee kabisa tuzungumzie mtu unaye mpenda anapokufa.unajua ni kwanini nimezungumzia swala hili? Sababu mara nyingi watu wanaouliwa walikua ni vipenzi vya watu.wewe unafikiri watu hawa wanao uliwa mwisho wake ni nini?Je unafikiri damu za watu hawa waliouliwa wataacha kukuandama katika maisha yako? Je unafikiri kilio cha ndugu zake walioachwa wapweke kitaanguka chini bila kukuzuru? Hakika nakwambia hautaishi kwa raha hata siku moja kwani hakuna dhambi kubwa kama ya kuua.

Ebu fikiria umemuuwa kijana ambae ameoa karibuni,ni majonzi kiasi gani umesababisha kwa mke wake? Ebu jaribu kuwaza mzazi wako anauwawa wakati ukiwa form one nayeye ndio pekee unae mtegemea katika shule? Wewe unafikiri kilio cha watu hawa kitakuacha? Mzee chemsha bongo hayo mambo ni ya kawaida sana kule ukweni kwenu(upareni).
Sasa nini tufanye naacha swali hilo kwa wanablog mulijadili bila kusahau
Maandiko matakatifu ya mungu yanasema
usimuhukumu mwenzio kwani na wewe pia utaukumiwa kwa kipimo hichohicho.


Wakati mwingine tena wazee.

Tuesday, September 4, 2007

Tanzania kutoka utandawazi mpaka hari mpya

Naamka asubuhi nafungulia redio nakutana na taarifa inayazungumzia kuwa serikali imeamua kuanzisha shule za secondary katika kila kata,nilifurahi sana kwani ni kama ndoto,nikasema sasa taifa litakua limejikwamua katika swala la elimu,na watoto wa walala hoi wataweza kutoboa mpaka vyuoni sasa.lakini gafla kengele ya hatari ikaita kichwani mwangu,nikajiuliza hivi mpango huu wa kuanzisha shule katika kila kata sio kama utakua umeharakishwa sana? Maana ki msingi Taifa lipo katika hali tata kuhusu waalimu,iweje leo serikali itake kuwa na shule za kata?

Ni busara kama serikali ingeamua kuweka swala hili kama mpango mkakati wa muda mrefu na sio kukurupuka,kwa mtazamo wangu mimi niliona kuwa serikali ingeanza na mpango wa kupeleka waalimu shule kwa muda wa miaka mitano,hapa namaanisha wangeweza kuwa na waalimu waliofuzu wakutosha alafu swala la kujenga shule lifuate.

Kutokana na kukurupuka serikali inapeleka wanafunzi wa form six kwenye mafunzo ya uwalimu kwa mwezi mmoja,matokeo yake tunakuwa na waalimu ambao

hawajajifunza vizuri hasa mbinu za ufundishaji na jinsi ya kuishi na
wanafunzi,unajua nini kinafuata hapo,ni kuwa na wahitimu ambao hawataweza kutuwakilisha kimataifa,pia tutapata madaktari feki,wahasibu wakughushi,na wataalamu wa kusuasua.

Kabla sijatoka kitandani nasikia matokeo ya kidato cha sita yametoka,nikapata mshituko kwani nina ndugu zangu waliohitimu mwaka huu,kabla sijakaa sawa wanatangaza mwaka huu wanafunzi wamefaulu kwa kiwango kidogo ukifananisha na mwaka jana,nikafikiria sasa ule mpango wa serikali kuanzisha shule za kata utasaidia kufaulisha wanafunzi au ndio utadidimiza? Jibu tunalo wenyewe!

Wakati naendelea kujiuliza nikapata kitu kingine,kuwa waalimu wenyewe wanaokwenda kwenye hiyo crash program ni kati ya wanafunzi walioshindwa kidato cha sita,swali je kama mtu anaekwenda kusomea uwalimu alifeli atawezaje kumfundisha mtu akafaulu? Siku hizi utaalamu wa uwalimu uchukuliwa na watu ambao wameshindwa kujiunga sehemu zingine,wanafanya uwalimu ni sehemu ya kukimbilia,kwa mtindo huu tutafika? Serikali itaweza kufikia malengo ya MKUKUTA? Jibu sijui….

Naendelea kutafakari hali halisi ya uchumi kwa jamii nzima nashindwa kupata jibu,hali ni mbaya kwa taifa nzima,watu hawana pesa,ajira zimekuwa dhahabu,kuna wakati nikajiuliza hivi hali hii ya uchumi itadumu mpaka lini? Au ndio hari na kasi mpya? Maana mfumuko wa bei ndio huwooooo!!!! Kodi za bidhaa ndio hatuelewi hatima yake kwani kila kukicha vitu havishikiki,lakini kwasababu hii ni nchi ya kitu kidogo watu wanamezea na siku zinakwenda.

Kelele za viongozi hivi sasa ni kuhusu kujiajiri (ujasiriamali),viongozi hao ambao wanapiga kelele za ujasiliamali hawajawahi kuwa hata na kibanda cha kuuza nyanya,ni wepesi sana kuimba ujasiliamali lakini kuutekeleza nikasheshe,ujasiliamali hausimami wenyewe kama baadhi ya vitu kama sera nzuri za nchi,kodi zinazovutia kwa biashara zinazoanza,Elimu itolewe juu ya ujasiliamali,kuzuia vitu kutoka nje visilete ushindani na uwepo wa taasisi za fedha ili kuwezesha wajasiliamali,vitu hivi vikiwepo basi tunaweza zungumzia ujasiliamali.

Kuna mtu mmoja aliniambia aisee serikali ya sasa mikopo njenje,nikamuuliza mikopo ipi hiyo? Akasema si ya kikwete? Ni kamuuliza umeshachukua hapo? Akasema ipoo! Ipo umepata? Hapana,hiyo ndio nchi ya watu wadogo.

Mzee zamani kulikua na kodi ya kichwa watu walikuwa wanaacha familia zao na kukimbilia porini,ilikuwa inatenganisha familia haswa,kipindi hicho watu walikuwa sio wavumilivu na sehemu za kukimbilia zilikuwepo,sasahivi kodi zilizopo hazina tofauti na hiyo kwani mtu anapokea mshahara ambao ukiuangalia kodi ni kiasi kikubwa mpaka unakata tamaa,kama haitoshi basi mtu huyohuyo anatozwa kodi katika bidhaa atakazonunua,sio hiyo tu nauli za daladala nazo zipo kwenye chati,kwa mishahara yetu ya koma moja ndani ya wiki mbili hauna pesa unageuka kuwa ombaomba,sasa unajiuliza hivi nafanya kazi au nafanyia watu kazi? Je mtu huyu akiamua kukimbilia nje ya nchi atakuwa ametofautiana na aliyekuwa anakimbia kodi ya kichwa? Jibu tunalo.

Maisha ya watanzania wengi ni ya kusuasua,ndio maana unakuta mtu anamiaka juu ya thelethini bado hajaoa,sio kama hapendi kuoa bali mambo hayajakaa sawa,swali ni lini mambo hayo yatakaa sawa? Watu haohao wanakufa sababu ya umri na kuziacha familia zao changa zinateseka.tulio wengi mamboyanaanza kuwa ya afadhali tukiwa na umri wa kuitwa babu,mtu huyohuyo unakuta hajatoka kwa baba na mama wakati nchi zilizoendelea mtoto anapokwenda chuo kikuu akirudi uko anaanza kujitegemea mwenyewe wala hatopokelewa nyumbani.,hapo ndio utajua unaishi katika nchi hipi? Kwanini tusikimbilie marekani kutafuta maisha? Unafikiri waliokwenda uko wakina ndesanjo,egidio,liganga,john selemani na ibra watarudi tena wakikumbuka jua kali la bongo?.....ngoja tuwasubiri.au uanasemaje mzee chemsha bongo?

Nikiwa mdogo baba yangu aliniambia uku akiwa amekaza meno na macho kuwa nisioneshe hisia zangu wakati wote,iwe nina tatizo au raha,mara ya kwanza nilishindwa kumuelewa alikua anamaanisha nini lakini nilikuja kumwelewa baada ya kujua kuwa mara nyingi tamaduni zetu zinawafanya wanaume kuwa wastahimilivu,na wala sikumbuki ni lini baba aliwahi kunikumbatia na kunipongeza kwa jambo zuri nililowahi kutenda,sasa unaweza kuona ni jinsi gani hata mzazi anamlea mototo wake katika hali ya shida kwani yeye mwenyewe anatambua kabisa kuwa lazima tutapata tabu uko mbeleni,lakini hii sio kawaida kwa nchi za wenzetu.

Itafikia wakati tutahita kumjua mchawi wa nchi yetu ni nani? Na pindi tukimjua lazima tutamfanyia kazi ipasavyo,kwani mtu huyu ni mbaya sana katika maendeleo ya nchi hii yetu ya kitu kidogo.

Tunatambua kuwa uwongozi ni kazi nzito sana tena ni ya kubeba dhamana ya walalahoi walio wengi,hivi unafikiri mtoto mdogo ukiwa unamchapa kila siku bila sababu mwisho wake unafikiri ataendelea kuvumilia tuu? Ipo siku atachoka na kuamua kukurudishia,vivyo hivyo hata watanzania watachoka na kuamua kuchukua maamuzi yatakayo shangaza dunia,siombei iwe hivyo lakini huo ndio ukweli mzee.

tuonane wakati mwingine mzee mkubwa.

why i hate visiting rich people

Question: What would you like to have? Fruit juice, Soda, tea, Chocolate,
Milo or Coffee?
Answer: Tea Please.

Question: Ceylon Tea, Herbal Tea, Bush Tea, Honey Bush Tea, Ice Tea or Green Tea?
Answer; Ceylon Tea.

Question: How would you like it? Black or White?
Answer: White.

Question: Milk, Whitener or Condensed milk?
Answer: With milk

Question: Goat milk, camel milk or Cow milk?
Answer: With cow milk please.

Question: Milk from freeze land cow or Afrikaner cow?
Answer: UM!! I’ll like it black.

Question: Would you like it with sweetener, sugar or honey?
Answer: with sugar.

Question: Beet sugar or cane sugar?
Answer: cane sugar.

Question; white, brown or yellow sugar?
Answer: Forget about tea just give me a glass of water instead.

Question: mineral water or still water?
Answer: Mineral Water.

Question: Flavored or non- flavored?
Answer: Never mind, I’ll rather die of thirst!

NYAMBAFU.